Nuru FM

DC Linda aiagazi Mafinga Mji kujenga uwanja wa michezo bajeti ijayo

20 November 2024, 6:13 pm

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Linda Salekwa akizungumza katika baraza la Madiwani Halmashauri Mafinga Mji. Picha na Hafidh Ally Rajuun

Na Hafidh Ally Rajuun

Mkuu wa wilaya ya Mufindi Dkt. Linda Salekwa ameiagiza Halmashauri ya Mafinga Mji kutenga fedha katika bajeti ijayo ili kujenga uwanja wa michezo.

DC linda ameyasema hayo leo katika baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mafinga Mji  leye kujadili taarifa za Utekelezaji Kazi za Maendeleo kwa kila kata kwa kipindi cha Robo ya Kwanza July Septemba 2024/2025 na kuongeza baraza hilo lina jukumu la kutenda zaidi ya Milioni 20 ambazo zilishapitishwa katika vikao vyao ili kuwa na viwanja vya michezo ambavyo vitasaidia kuibua vipaji vya vijana kutoka Mafinga.

“Mimi nawashauri Madiwani watenge bajeti kujenga kiwanja kizuri cha michezo kwani itasaidia mji wa mafinga kupendeza hasa ukiangalia kwa sasa tuko kwenye mchakato wa kujenga barabara za lami katika maeneo yote, na hizo timu za ligi kuu zinaweza kuja hapa iringa kutumia viwanja vyetu na kuwaona vijana wetu” alisema Linda

Sauti ya DC Linda

Aidha Mh. Linda ameiongeza Halmashauri ya Mafinga mji kwa kuibuka na tuzo tatu katika mashindano ya shirikisho la michezo ya serikali za Mitaa ambapo walifanikiwa kuchukua tuzo ya uimbaji wa ngoma na tuzo za Kwaya, na tuzo ya Mpira wa wavu upande wa wanawake.

Kwa upande wake Afisa Michezo mwandishi wa Mafinga Mji Henry Kapela amesema kuwa wamepokea maagizo hayo na tayari walishatenga kiwanja katika eneo la changarawe na wanaanza mchakato wa kutenga bajeti.

Sauti ya Afisa Michezo

Henry amesema kuwa pia watajifunza katika halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kujua hatua ambazo walizifanya mpaka wakajenga uwanja wa KMC Komplex.

“pia tutashiririkiana na watalaamu wa majengo ili kupata ramani ya kisasa yenye michoro ya uwanja ambao kama Halmashauri tukiridhika nao tutaupitisha katika vikao vijavyo vya bajeti” Alisema Henry

Awali Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mafinga Mji Reginant Kivinge alisema kuwa ni michezo ni agenda nzuri ambayo itasaidia vijana watakaozalishwa kupitia mashindano mbalimbali kama UMISETA na UMITASHUMTA kuitangaza Halmashauri kwa kutoa vijana wenye vipaji.