Milion 600 kujenga sekondari ya Igowole Mufindi
21 October 2024, 11:35 am
Na Fredrick Siwale
Serikali imetenga zaidi ya milion 600 katika shule ya sekondari Igowole wilaya ya Mufindi mkoani Iringa ili kuboresha miundombinu ya elimu.
Hayo yamezungumzwa Katika mahafali ya 34 katika Shule ya Sekondari Igowole na Afisa elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Bw. Daniel Mapilya alipokuwa mgeni rasmi kwa kumwakilisha Mh. David Mwakiposa Kihenzile Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara na kuongeza kuwa hatua hiyo imesaidia kukuza ufaulu na taaluma katika shule hiyo.
Aidha Mapilya amesema kuwa Mbunge Kihenzile atakarabati vyumba viwili vya shule ya sekondari igowole kwa asilimia mia moja.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Igowole Innocent Mgoda katika risala yake kwa mgeni rasmi,amesema Shule hiyo inafanya vizuri katika taaluma huku wakiishukuru serikali kwa kufanikisha ujenzi wa bwalo shuleni hapo.
MWISHO