Manispaa ya Iringa yatenga Mil 918 kuwakopesha vijana
24 September 2024, 9:30 am
Mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmshauri hapa Nchini imetajwa kuwa mkombozi kwa wanufaika huku Serikali ikisubiriwa kutoa tamko juu utaratibu wa utolewaji wake.
Na Hafidh Ally
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imetenga zaidi ya shilingi milioni 918 ambazo zitatumiwa kwa ajili ya kuwakopesha vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
Hayo yamezungumzwa na Mstahiki Meya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ally Ngwada na kuongeza kuwa fedha hizo zipo na wanachosubiri ni maelekezo kutoka serikalini namna ya kuzitoa katika makundi hayo.
Aidha Ngwada amebainisha kuwa watatoa ushirikiano kwa vijana na ambao wanataka mikopo kwa kushirikiana na ofisi za maendeleo ya jamii na ofisi za Vijana.
Katika hatua nyingine Meya huyo amebainisha kuwa kama makundi hayo yanaona kuna changamoto kuhusu utoaji wa mikopo ni vyema wakafika katika ofisi za halmashauri ili zitatuliwe.
MWISHO