Nuru FM

CHADEMA Iringa kutekeleza azimio la kuandamana

16 September 2024, 1:42 pm

Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la IRINGA Mjini Frank Nyalusi akizungumzia azma Yao ya kufanya maandamano. Picha na Ayoub Sanga

Na Godfrey Mengele

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Iringa Mjini kupitia Mwenyekiti wa jimbo hilo, Frank Nyalusi kimetuma salamu kwa Jeshi la Polisi kufuatia azimio la kuandamana lililotolewa na kamati kuu ya chama hicho.

Nyalusi ameyasema hayo katika mkutano wa chama uliofanyika kata ya Igumbilo Manispaa ya Iringa, ukilenga kutoa Elimu kwa wananchi wa kata hiyo, kuelekea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika November 2024.

Amesema kuwa lazima watatekeleza matakwa ya kufanya maandamano hayo tarehe 23 kudai haki za waliotekwa huku akiwaasa Jeshi la Polisi kutodhihaki maisha ya watanzania wanaopotea.

MWISHO