Mapesa: Miundimbunu bora ya shule fursa kwa watoto kusoma
4 September 2024, 12:13 pm
Na Joyce Buganda
Wazazi na walezi wa kijiji cha Kisilwa Kata ya Mahuninga Wilaya ya iringa wamepongezwa kwa kuwa na muamko wa kuwaendeleza watoto wao shule pindi wanapomaliza darasa la saba.
Hayo yamezungumzwa kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha kisilwa na Afisa tarafa wa Idodi Makala Mapesa na kuongeza kuwa kipindi cha nyuma wazazi walikuwa wanawaozesha watoto wao mara baada ya kumaliza darasa la saba lakini baada ya serikali kuboresha moundombinu ya shule wazazi wamekuwa na mwamko wa kuwapatia elimu watoto wao.
Naye Diwani wa kata ya mahuninga Benitho kisogole amesema Zaidi ya shilingi bilioni 1 zimeletwa kwenye kata hiyo kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwemo elimu.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Makifu Jailos Mwakavindi amesema shilingi million 260 zimeletwa shuleni hapo kwa ajili ya ujenzi wa bweni pamoja na ujenzi wa vyoo.
MWISHO