Nuru FM

CWT Iringa wanunua gari kurahisisha utendaji kazi

3 September 2024, 9:50 am

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Kheri James akiwa na viongozi wa CWT wakati wa uzinduzi wa Gari la walimu. Picha na Joyce Buganda.

Na Joyce Buganda

Mkuu wa Wilaya Iringa Kheri James amewapongeza Chama cha walimu Tanzania mkoa wa Iringa kwa mafanikio ya kununua gari kwa ajili ya shughuli mbalimbali.

Pongezi hizo zimetolewa wakati wa kutambulishwa kwa gari lililonunuliwa kwa michango ya wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Manispaa ya Iringa na kusema kuwa Halmashauri hiyo ina walimu wengi hivyo uwepo wa gari hilo ni itasaidia kuwahudumia kikamilifu wanachama wake.

Sauti ya DC Kheri

Kwa upande wake Kaimu Katibu wa Chama cha walimu Iringa Manispaa Dominic Boniphace ameeleza kabla ya ujio wa gari hilo changamoto walizokuwa wakizipitia ni pamoja na baadhi ya walimu kushindwa kuhudhuria katika matukio ya kijamii.

Sauti ya Dominic

Naye mwenyekiti wa chama cha walimu manispaa ya Iringa Frank Lupeke amewashukuru walimu waliokubaliana kununua gari hilo ili litumike katika masuala ya kijamii, kitaaluma na ziara.

Sauti ya Frank

Baadhi ya walimu waliofanikiwa kuhudhuria katika utambulishwaji huo wamesema gari hilo litawasaidia kushiriki katika matukio mbalimbali ya furaha na huzuni pamoja na kuwawezesha kusafiri kwa wingi kwenda katika mafunzo.

Sauti ya Walimu