Nuru FM

Wafanyabiashara Iringa walalamikia mitaji kufa, chanzo kushuka kwa bei za bidhaa

5 August 2024, 11:19 am

Wafanyabiashara wa soko kuu Iringa wakiendelea na majukumu yao. Picha na Naida Athanas

Na Naida Athanas

Kushuka kwa bei za bidhaa mbalimbali imetajwa kuwa sababu ya kushuka Kwa mitaji ya wafanya biashara Manispaa ya Iringa.

Wakizungumza na NURU FM  baadhi ya wafanya biashara wameeleza kufungwa kwa mipaka ya nchi, kupepelekea mazao hasa mchele, unga, vitunguu na mahindi kuwa mengi huku  mzunguko wa biashara ukiwa mdogo na kupelekea walaji kunufaika.

Sauti wafanyabiashara

Kwa upande wao baadhi ya  wanunuzi wa bidhaa hizo wanaeleza kupata unafuu wa maisha kwa sasa kutokana na bei za bidhaa kua chini tofauti na hapo nyuma bei zilikuwa juu.

Sauti ya Wanunuzi

Nuru Fm tililazimika kuwafikia Wafanyabiashara wa vyakula Manispaa ya Iringa maarufu  Mamalishe Kujua hali halisi ya biashara  kufuatia baadhi ya bidhaa kushuka bei ikiwemo mchele ambapo wamesema biashara bado ni ngumu kutokana na wateja kuwa wachache hivyo wanalazimika kubadilisha kipimo cha chakula kila siku ili kuendeleza mtaji.

Sauti ya Mamalishe

MWISHO