Nuru FM

Mbunge Kabati akabidhi vitanda Zahanati ya Ng’ang’ange

30 July 2024, 9:01 am

Mbunge wa viti maalumu Mkoa WA Iringa Dkt. Ritta Kabati akikabidhi Msaada wa Vitanda. Picha na Halfan Akida.

Na Halfan Akida

Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Iringa, (CCM), Dr. Ritta Kabati ametekeleza ahadi yake ya kusaidia vitanda 3, Mablanketi pamoja na mashuka katika zahanati ya Ng’ang’ange iliyopo wilaya ya Kilolo.

Kabati amekabidhi vitanda hivyo wakati alipofanya ziara ya kikazi katika kata hiyo na kuongeza kuwa vitanda hivyo ni muendelezo wa kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN kwa namna anavyoboresha sekta ya afya Nchini.

Sauti ya Kabati

Aidha Kabati amebainisha kuwa ameamua kufanya ziara katika vituo vya afya, zahanati na hospitali zote mkoani hapa ili kujua changamoto zinazowakabili na namna ya kuzitatua.

Sauti ya Kabati

Kwa upande wake, katibu wa UWT wilaya ya Kilolo, Mariam Kasembe amempongeza mbunge Kabati kwa kutekeleza ahadi yake katika zahanati hiyo huku akiwataka viongozi na wadau wa maendeleo kuendelea kuwa na moyo wa kusaidia zaidi jamii.

Sauti ya Katibu UWT

Akipokea Msaada huo kwa niaba ya zahanati hiyo, Selina Makundi ambaye ni Afisa Muuguzi msaidizi amemshukuru mbunge Ritta Kabati kwa kutoa msaada huo kwa kuwa vitanda vilivyokwepo vilishakuwa chakavu.

Sauti ya Muuguzi

MWISHO