Nuru FM

Waziri Majaliwa aagiza kuondolewa madawati yasiyokidhi vigezo Iramba

8 July 2024, 8:14 pm

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika Ziara ya kikazi Wilaya ya Mufindi. Picha na Mwandishi wetu.

Na Mwandishi wetu.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, ameagiza kuondolewa kwa madawati yaliyopo katika shule ya sekondari ya Iramba Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa ambayo hayana eneo la kuhifadhi madaftari ya wanafunzi.

Waziri Majaliwa ametoa agizo hilo mkoani Iringa wakati akizindua shule ya wasichana ya Iramba baada ya kubaini kuna madawati ambayo hayana eneo la kuhifadhia madaftari ya wanafunzi licha ya dawati moja kugharimu kiasi cha shilingi elfu 50.

Sauti ya Majaliwa

Amesema Mh. Majaliwa amewataka viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kuhakikisha ujenzi wa shule ya Iramba unakamilika ili wanafunzi waanze kusoma kuanzia mwaka 2025.

Sauti ya Majaliwa

Ujenzi wa Shule hiyo unategemewa kugharimu kiasi cha Bilioni 1.78 mpaka kukamilika kwake, ukihusisha jengo la utawala (1) Madarasa (8) Ofisi (4), Maabara (1), Chumba cha TEHAMA (1) Nyumba za walimu (5), Bwalo la chakula (1) na Mabweni (4).

Mpaka sasa kiasi cha shilingi milioni 363.8 kimepokelewa ikiwa ni shilingi milioni 2.2 nguvu za wananchi na Halmashauri ya wilaya shilingi milioni 361.6.

MWISHO