Nuru FM

Nyalusi: Msigwa ameacha pengo CHADEMA

3 July 2024, 11:48 am

Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Iringa Mjini Frank Nyalusi akizungumzia kuondoka kwa msigwa Chadema. Picha na Fabiola Bosco.

Na Michael Mundellah na Naida Atannas

Siku chache baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa Peter Msigwa kujiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM, Uongozi wa Chadema Jimbo la Iringa Mjini umesema kuwa umempoteza kiongozi ambaye aliwasaidia kwa asilimia 65.

Akizungumza na Nuru fm kuhusu hali ya siasa ndani ya Chadema baada ya kuondoka kwa Msigwa, Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Iringa Mjini Frank Nyalusi   amebainisha kuwa watamkumbuka Msigwa kwani alikuwa kiongozi mwenye ushawishi katika chama chao.

Sauti ya Nyalusi

Aidha Nyalusi amesema kuwa wanachama wa CHADEMA wanatakiwa kuwa na umoja na ushirikiano kwa sasa ili kuongeza nguvu ya kisiasa baada ya kuondokewa kiongozi huyo.

Sauti ya Nyalusi

Kwa upande wao baadhi ya wananchi manispaa ya Iringa wamekuwa na maoni tofauti baada ya Msigwa kuhamia chama cha mapinduzi CCM.

Sauti ya Nyalusi

Msigwa alitambulishwa kuwa mwanachama mpya wa CCM, Juni 30, 2024, mbele ya wajumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho (NEC), katika kikao kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan.

MWISHO