Nuru FM

Mzava: Gombeeni nafasi za uongozi serikali za mitaa

28 June 2024, 7:44 pm

Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Godfrey Mzava akizungumzia kuhusu uchaguzi wa serikali za Mitaa. Picha na Adelphina Kutika.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hutumika kuwapata Viongozi wataoongoza wananchi wao kuanzia Ngazi ya Mtaa huku wananachi wakihimizwa kushiriki ipasavyo.

Na Adelphina Kutika

Wananchi wa Iringa Mjini wametakiwa kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu 2024.

Ushauri huo umetolewa na Kiongozi wa Kitaifa wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024, Ndg. Godfrey Mzava, alipokuwa akizungumza na wananchi katika eneo la Mwembetogwa, kata ya Makorongoni, Manispaa ya Iringa.

Sauti ya Mzava

Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa, Michael Semundu, ameeleza kuwa halmashauri ya wilaya imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia mikutano ya hadhara na vyombo vya habari ili kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika uchaguzi huo.

Sauti ya Semundu

Daudi Yassin, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, amewahimiza wananchi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ili kuchagua viongozi wenye uwezo na weledi ifikapo mwezi October.

Sauti ya Mwenyekiti CCM