Nuru FM

Mwenge wa uhuru 2024 wazindua kituo cha mafuta cha ASAS energies

25 June 2024, 11:36 am

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Kheri James, Mkurugenzi wa Kampuni ya mafuta ya ASAS Energy Ahmed Abri na Kiongozi Mkuu wa mbio za mwenge Kitaifa Godfrey Mzava wakifuatilia Mradi wa kituo Cha Mafuta. Picha na Adelphina Kutika.

Kiongozi wa mbio za mwenge ameridhia kuzindua Mradi wa ujenzi wa kituo Cha Mafuta Cha ASAS Energy ili kisaidie upatikanaji wa huduma ya nishati.

Na Adelphina Kutika

Mwenge Wa Uhuru 2024  Umezindua Kituo Cha Mafuta Cha Asas Energies Ltd kilichopo Kata ya Igumbilo Manispaa ya iringa Kilichogharim Shilingi Bilion 1

Akizindua Mradi huo Godfrey Mzava, ambaye ni kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa, amesisitiza umuhimu wa uwekezaji huo utachochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Sauti ya Mzava

Aidha amempongeza Mfanyabiashara huyo Ahmed Abri kwa kujitolea kwake katika kukuza sekta ya mafuta na gesi nchini Tanzania, na kuonyesha jinsi ujenzi wa kituo hicho utakavyoongeza fursa za ajira na kuimarisha uchumi wa eneo la Igumbilo.

Sauti ya Mzava

Kituo cha Mafuta cha Asas pia kinajumuisha huduma mbalimbali kama vile mikahawa na maduka madogo ambayo yatasaidia kuongeza kipato cha wenyeji na kuboresha huduma za kijamii.

Hii ni hatua muhimu katika kukuza biashara na kuvutia wawekezaji zaidi katika eneo hilo lenye uwezo mkubwa wa kiuchumi.

Uzinduzi huu unakuja wakati ambapo sekta ya mafuta nchini Tanzania inapanuka na kuimarika.

Ameongeza kuwa , kituo hicho kinatoa fursa kwa watumiaji wa mwisho kupata huduma bora za mafuta kwa bei za ushindani, hivyo kuchangia katika kuboresha maisha ya wananchi.

Kwa kuzingatia umuhimu wake katika kuchochea maendeleo ya eneo la Igumbilo na maeneo ya jirani, uzinduzi wa Kituo cha Mafuta cha Asas unaweza kuchukuliwa kama mfano mzuri wa jinsi uwekezaji wa sekta binafsi unavyoweza kusaidia katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu ya kitaifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya ASAS Energy Ahmed Abri amesema kuwa ujenzi wa kituo hicho umegharimu shilingi billion 1 huku wakitarajia kutoa huduma Bora za nishati kwa wananchi.