Wanahabari kutumia kalamu zao kuhusu malezi bora
19 June 2024, 10:44 am
Na Adelphina Kutika
Waandishi wa habari wa redio jamii mkoani Iringa wametakiwa kutumia kalamu zao kuandika na kuelimisha jamii ili kuleta mabadiliko chanya kwa mtoto na taifa kwa ujumla.
Hayo yamebainishwa katika ufunguzi wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu Program Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) mjumbe wa bodi ya UTPC na mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Iringa (IPC) Ndugu Frank Leonard ambapo amesema kuwa wandishi wana wajibu wa kuhakikisha wanaelimisha jamii ili kuondokana changamoto ya malezi.
Mratibu Programu ya (PJT-MMMAM) Mkoa wa Iringa ambae ni Mkufunzi kutoka Shirika la Development of Youth Disabled & Children Care (IDYDC) Ruben Magayane amesema malengo ya serikali kupitia mafunzo hayo ni kutoa elimu ya malezi ,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kwa wazazi na walezi kupitia waandishi wa habari.
Mkufunzi wa mafunzo hayo na mwandishi Mchechemuzi wa habari za watoto ambae pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Makutano TV Bi .Tukuswiga Mwaisumbe amesema kwa sasa kwenye taaluma ya waandishi wa habari utandawazi umewapa nafasi kubwa watu wasio na taaluma kuandika habari bila kuzingatia maadili.
MWISHO