Nuru FM

Mkoa wa Iringa kinara kwa udumavu

10 June 2024, 1:59 pm

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba akizungumzia kuhusu Hali ya udumavu Mkoani Iringa na namna ya kupambana nao. Picha na Joyce Buganda

Licha ya serikali kufanya jitihada kumaliza tatizo la udumavu nchini, mkoa wa Iringa umebaki kuwa mkoa unaoongoza kwa tatizo la udumavu nchini.

Na Joyce Buganda

Watoto wenye umri wa miaka 0-5 mkoa wa Iringa wanakabiliwa na changamoto ya udumavu sawa na asilimia 56.9.

Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Peter Serukamba ambapo ameeleza kuwa mpaka sasa kiwango cha udumavu ni kikubwa huku mkoa wa Iringa ukishika nafasi ya kwanza nchini ambapo amewataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao kupima hali ya udumavu.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa

Serukamba ameeleza kuwa ili kukabiliana na changamoto hiyo mkoa umeanzisha kampeni ya siku nne kwa lengo la kutathimini na  kujua maeneo yanayokabiliwa zaidi ma changamoto ya udumavu.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa

Hata hivyo serikali ya mkoa wa Iringa imeagiza kila halmashauri kutenga kiasi cha shilingi elfu moja kwa kila mtoto shuleni lengo likiwa ni kutokomeza udumavu.

Mkoa wa Iringa unaongoza kuwa na tatizo la udumavu kwa asilimia 59.9, Njombe asilimia 50.4 ukifuatiwa na Rukwa asilimia 49.8.

MWISHO