Wananchi walalamikia vilabu vya pombe kuzunguka shule ya Mlamke
4 June 2024, 10:55 am
Shule ya Sekondari Mlamke inakabiliwa na ukosefu wa uzio jambo linalopelekea wanafunzi kupata kero kutokana na uwepo wa vilabu vya pombe pembezoni mwa shule hiyo.
Na Adelphina Kutika
Wananchi wa kata ya Ilala katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wameiomba serikali kuweka uzio katika shule ya Sekondari Mlamke ili kuimarisha mazingira Bora ya kujisomea Kwa wanafunzi.
Azungumza Kwa niaba ya wananchi Diwani wa kata ya Ilala Conradi Mlowe katika mkutano wa hadhara mbele ya Mkuu wa wilaya Ndugu Kheri James amesema shule ya Mlamke inakabiliwa na ukosefu ya uzio Hali inayopelekea wanafunzi kushindwa kusoma Kwa utulivu kutokana na kuzungukwa na vilabu vya pombe.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada amesema kama Halmashauri wameweka mkakati wa kuhakikisha wanaboresha shule kongwe zote ukiwemo kuweka mpango wa kuweka uzio wa shule hiyo.
Mhe.Kheri James akiwa katika mkutano wa hadhara katika kata hiyo amewahimiza wananchi kuhakikisha wanashiriki katika kupanga na kuamua katika suala la maendeleo.
Kheri James ameeleza kuwa Serikali imejipanga kupambana na rushwa, Uzembe, Urasimu na Utoro kazini ili watumishi wa umma waweze kuwajibika kikamilifu na Wananchi waweze kuhudumiwa kwa wakati na ufanisi.
Katika ziara hiyo Komred Kheri James ameeleza kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi katika miradi ya Elimu, Afya, Nishati na Maji ili kila Mwananchi aweze kuipata huduma bora katika eneo alilopo.