TCCIA yaiomba TRA kuwapunguzia wafanyabiashara kodi
23 May 2024, 12:27 pm
Licha ya wafanyabiashara kufanya kazi zao kwa mazignira rafiki Bado kumekuwa na changamoto ya kukadiriwa Kodi kubwa.
Na Joyce Buganda
Wafanyabiashara mkoani Iringa wameilalamikia mamlaka ya mapato Tanzania TRA kuwatoza kodi kubwa hasa wanaposafirisha bidhaa zao kutoka mikoa ya jirani.
Wakizungumza wakati wa ziara ya Rais wa chemba ya wafanyabiashara, wenye viwanda na wakulima TCCIA wafanyabiashara hao wamesema wanakumbana na changamoto nyingi ikiwemo hiyo ya TRA wanasema VAT imekuwa ikiwatesa jambo ambalo limekuwa likiwashusha kibiashara.
Naye Rais wa Chemba ya wafanyabiashara, wenye viwanda na wakulima TCCIA Vicent Minja amesema wanaangalia maendeleo ya chemba kuanzia wilayani mpaka ngazi ya mkoa , kuangalia fursa zilizopo katika mikoa lakini pia kukusanya changamoto zilizopo na kuzifanyia kazi.
Awali Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa iringa Edmund Mkwawa amesema wana mpango wa kukaa kikao na wafanyabiashara kuanzia wilayani mpaka ngazi ya mkoa ili kuendelea kuiinua taasisi hiyo.
Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba amesema kuwa serikali ya mkoa itakuwa tayari kushirikiana na chemba hiyo ya wafanyabiashara kuleta mafanikio makubwa kwa kundi hilo.
MWISHO