TRA kutumia mbio za mwenge kutoa elimu ya kodi
3 April 2024, 9:39 am
Uwepo wa Mwenge unasaidia kuwakutanisha watu wa kada mbalimbali ambao wanatakiwa kupatiwa elimu ya kodi ili kuongeza fedha za kukuza miradi ya maendeleo.
Na Mwandishi wetu.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema imejipanga kutoa elimu ya kodi kusikilza changamoto na kujibu maswali katika maeneo yote ambayo mwenge utalala
Kauli hiyo imetolewa na Afisa mkuu wa usimamizi wa kodi kutoka Makao Makuu, Hamady Mteri katika uzinduzi wa mbio za mwenge uliofanyika leo katika viwanja vya Ushirika vilivyopo Moshi mkoani kilimanjaro.
Amesema, uhusiano wa Mwenge una uhusiano mkubwa na kodi kwani ukimbizaji wa mbio za mwenge unaenda sambamba na uwekaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo ambapo utekelezaji wake utahitajia fedha ambapo kodi ndio chanzo kikuu cha pato la taifa.
Awali, Katibu wa waendesha bodaboda mkoani hapo, Rashid Omary aliishukuru TRA kwa kushiriki katika mbio za mwenge na kuwaomba wananchi kufika katika banda la TRA kwa lengo kujifunza mambo mbali mbali ya kodi, huku Modistus Malya akisema kodi ni maendeleo hivyo kuwataka Wananchi wanaofanya biashara kuilipa kwa maendeleo ya taifa.