Watendaji manispaa ya Iringa waagizwa kutatua kero za machinga
21 March 2024, 10:19 am
Changamoto za machinga zinatakiwa kutatuliwa ili kukuza uchumi wa mkoa wa Iringa
Na Joyce Buganda
Watendaji wa halmashauri ya manispaa ya Iringa wameagizwa kushirikiana kutatua tatizo la machinga ili kuleta maendeleo ya mkoa.
Agizo hilo amelitoa leo mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba wakati akimwapisha mkuu wa wilaya ya Kilolo na kuhimiza viongozi wote washikamane usiku na mchana kufanya kazi za serikali ili kuuweka mkoa wa Iringa kwenye mstari ulionyooka.
Joachim Nyingo ni mkuu wa wilaya mpya wa wilaya ya Kilolo amesema anamshukuru mhe. Rais kwa kumuamini na kumpeleka wilaya ya Kilolo na kuahidi kuitumikia wilaya hiyo kwa uadilifu.
Kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya Kilolo mwnyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo Ana Msola amesema viongozi na wananchi watahakikisha wanaendeleza ushirikiano ili kuleta maendeleo .