Nuru FM
Wanafunzi 130 Tosamaganga warudishwa nyumbani kwa siku 7
26 November 2020, 6:54 am
Wanafunzi 130 wa shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilayani Iringa wamerudishwa nyumbani kwa siku saba hadi watakapolipa shilingi elfu 35 kila mmoja baada ya kushiriki vurugu zilizosababisha uharibifu wa mali za shule wakigomea tarehe ya kuanza mtihani wa mwisho wa muhula.
Hatua hiyo imefikiwa na Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela pamoja na uongozi wa shule hiyo ya Tosamaganga baada ya wanafunzi hao wa kidato cha tano na sita kuvunja vioo vya madarasa kuharibu ofisi ya walimu na maktaba baada ya kuthibitishwa na Mwalimu Kalongelo ambaye ni makamu mkuu wa shule hiyo.