Nuru FM

Recent posts

21 May 2022, 11:28 am

Wafanyakazi wa Nuru Fm Watoa msaada kwa wafungwa Iringa

Wafanyakazi wa Redio Nuru fm wakishirikiana na watuma salamu Mkoa wa Iringa wamewatembelea wafungwa wa Gereza la iringa manispaa na kukabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali. Wakizungumza wakati wa kukabidhi mahitaji hayo yakiwemo mablanketi, mashuka, nguo, mafuta ya kupaka, sabuni za…

21 May 2022, 11:16 am

Wakwamishaji miradi Kigoma kukiona

Baraza la madiwani Halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji limeazimia kwa kauli moja kuchukulia hatua kwa viongozi wa wafanyabiashara wanaokwamisha mpango wa ujenzi na maboresho ya masoko ya Kigoma na Mwanga. Akiwasilisha ajenda maalum ya kujadili ujenzi wa masoko hayo…

21 May 2022, 11:14 am

Wauzaji nishati ya gesi wahimizwa matumizi ya mizani

Wauzaji na wasambazaji wa nishati ya gesi wametakiwa kuhakikisha wanakuwa na mizani ya kupimia kiwango stahiki cha gesi kama sheria inavyoagiza. Wito huo umetolewa na Meneja wa mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na Maji (EWURA), Kanda ya kaskazini…

20 May 2022, 7:48 am

Machinga Kutungiwa Sheria Ya Kuwalinda

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula amesema Serikali imeanza mchakato wa kutunga Sheria ya kuwalinda wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama ‘machinga’. Dkt. Zainab ametoa kauli hiyo  jijini Dodoma Mei 19, 2022…

20 May 2022, 7:40 am

Bajeti ya wizara ya Ulinzi yapita

Bunge limeidhinisha bajeti ya Sh trilioni 2.7 ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa (JKT) bungeni mjini Dodoma . Akiwasilisha bajeti hiyo jana ,  Waziri wa Ulinzi, Stergomena Tax, amesema katika Mwaka wa Fedha…

20 May 2022, 7:37 am

Profesa Lipumba amtabiria ushindi Rais Samia 2025

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba amesema anavutiwa na utendaji kazi wa Rais Samia Suluhu Hassan, hasa kutokana na kuwa msikivu kwa makundi mbalimbali. Lipumba ameyasema hayo wakati wa mkutano wa hadhara katika uwanja wa Ali Hassan…

20 May 2022, 7:35 am

Umoja wa Ulaya waruhusu kuendelea kununua gesi kutoka Urusi

Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya imeziruhusu nchi wanachama kuendelea kununua gesi kutoka Urusi lakini bila ya kukiuka vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Urusi baada ya nchi hiyo kuimavia Ukraine. Hata hivyo Halmashauri hiyo inazishauri nchi wanachama kutofungua akaunti za sarafu…

20 May 2022, 7:13 am

Simba SC yatangaza mpango wa ASFC

Uongozi wa Simba SC umetangaza rasmi kuweka kambi jijini Mwanza kwa ajili ya mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ utakaowakutanisha dhidi ya Young Africans Jumamosi (Mei 28), katika Uwanja wa CCM Kirumba. Simba SC imetangaza rasmi…