Nuru FM

Wafanyabiashara Soko la Mashujaa waomba Mikopo

10 April 2026, 08:43

Wafanyabiashara wa soko la Mashujaa wakimsikiliza Mbunge wao Mh. Villa. Picha na Fredrick Siwale

Na Fredrick Siwale

Wafanyabiashara wa Soko la Mashujaa Halmashauri ya Mji Mafinga wameiomba serikali kuwapatia Mikopo ili waweze kukuza mitaji yao.

Akizungumza na Nuru FM Mwenyekiti wa Soko la Mashujaa Bw. Devick Kihindo amesema kuwa wajasiriamali wengi wanatamani kupata mikopo ila bado hawajajua utaratibu wa kunufaika nayo.

Sauti ya Mwenyekiti

Naye Diwani wa Kata ya Boma Mh. Baraka Kisakanike Amekiri kuwepo kwa changamoto ya Mitaji kwa wajasiriamali wengi huku akibainisha kuwa tayari serikali imeweka utaratibu wa kunufaika na mikopo ya Halmashauri.

Sauti ya Kisakanike
Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mh Villa akizungumza na Wajasiriamali katika soko la Mshujaa.

Naye Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini Mh. Dickson Lutevele VILLA amesema kuwa wanaotaka mikopo lazima wawe kwenye vikundi vilivyosajiliwa na kwa kuwa wapo katika maeneo ya biashara watapewa kipaumbele.

Sauti ya Villa

Aidha Mh. Villa amesema kuwa baadhi ya wajasiriamali wanaogopa kufuata utaratibu wa kuchukua Mikopo ya Halmashauri na badala yake wanachukua mikopo ya kausha damu ambayo inakuja kuwaletea shida hapo baadaye.

Sauti ya Villa