Nuru FM
Nuru FM
10 April 2026, 09:09

Machinjio hiyo imetajwa kuwa msaada katika kuzingiatia afya za wananchi wa Kijiji hicho.
Na Joyce Buganda
Wananchi wa kijiji cha ng’uruhe Kilichopo wilaya ya kilolo wameshukuru shirika la African Exchange Development kwa kujengewa machinjio ya kisasa itayorahisisha shughuli za uchinjaji wa nyama.
Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamelishukuru shiriki hilo kwa kuwaletea machinjio hayo ya kisasa kijijini hapo ambapo awali hawakuwa na machinjio rasmi jambo lililohatarisha usalama wa afya zao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mipango na Fedha wa kijiji cha ng’uruhe Bw. Israel Magelenge amesema hapo awali walikuwa wanakabiliwa na ukosefu wa sehemu salama na yenye viwango bora vya uchinjaji hali iliokuwa ikiathiri ubora wa nyama pamoja na afya kwa walaji.
Naye Mwenyekiti wa Shirika la African Exchange Development Mwalimu Shadrack Nyaulingo amesema mradi huo ni sehemu ya juhudi za kuboresha maisha ya wananchi kupitia miradi ya maendeleo inayogusa mahitaji ya msingi ya jamii.
Machinjio hayo Yanatarajiwa kuwa chachu ya maendeleo ya uchumi kwa wakazi wa ng’uruhe hasa kwa wafugaji na na wafanyabiashara wa nyama huku wakichangia pia kuboresha hali ya afya kwa jamii kwa ujumla.