Nuru FM
Nuru FM
8 April 2026, 09:40

Meza hizo zimekabidhiwa ikiwa ni hatua ya kuwafanya wajasiriamali wafanye kazi zao katika mazingira rafiki.
Na Fredrick Siwale
Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini Mh. Dickson Lutevele VILLA ametimiza ahadi yake kwa kukabidhi meza 90 kwa Wajasiriamali wa Soko la Mashujaa.
Akizungumza na Wananchi wa Soko la Mashujaa Halmashauri ya Mji Mafinga, Mh Villa amesema amechukua uamuzi huo ikiwa ni sehemu ya ahadi yake ya kuwatua sinia kichwani Wajasiriamali hao ili waweze kufanya kazi katika eneo moja.
” Ndugu zangu nimeona kidogo nilichopata nanyi niwaletee ili mpate kutulia sehemu moja na kufanya biashara kwa utulivu sehemu moja badala ya kuzunguka mitaani.” Amesema Mh. Villa.

Naye Diwani wa Kata ya Boma Mh. Baraka Kisakanike amesema kuwa wajasiriamali waliokabidhiwa meza wanapaswa kufuata utaratibu wa serikali kwa kufanya biashara katika maeneeo yaliyotengwa.
Awali Mwenyekiti wa Soko la Mashujaa Bw. Devick Kihindo amemuomba Mbunge wa Jimbo Hilo, kuwatafutia eneo lingine la kufanya biashara kwani wajasairiamali wengi wanakosa maeneo ya kuendesha shughuli zao.
Kwa upande wao baadhi ya wajasiriamali waliokabidhiwa meza hizo wamemshukuru Mh. Mbunge kwa msaada huo huku wakiahidi kufanya biashara katika maeneo ambayo watapangiwa na serikali.
