Nuru FM

IDYDC yatatua changamoto ya maji Mangawe

3 April 2026, 10:26

Afisa Kutoka IDYDC akizngumza na wananchi wa Kijiji cha Mangawe kuhusu fursa ya kuunganishiwa maji ya Mkopo. Picha na Hafidh Ally

Wananchi wa Kijiji cha Mangawe Kilichopo Jimbo la Ismani wanatarajia kunufaika na Mradi wa Maji ya Mkopo usiokuwa na riba.

Na Hafidh Ally

Shirika lisilo la Kiserikali la Idydc Mkoani Iringa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira limefika Katika Kijiji cha Mangawe kwa ajili ya kuwapatia mkopo wa kuunganishiwa huduma ya maji safi wananchi wa eneo hilo.

Wakizungumzia Fursa hiyo baadhi ya wananchi wa Kijiji chA Mangawe Kata ya Ngang’oro Wilaya ya Iringa wamesema kuwa wengi wao wanashindwa kumudu gharama za kulipa maji kwa mkupuo  hivyo shirika hilo limekuja kuwa mkombozi na kutatua changamoto ya maji.

Sauti ya Wananchi Mangawe

Wananchi hao wamesema kuwa walikuwa wakikabiliwa na changamoto ya kutumia muda mwingi kutafuta huduma ya maji jambo ambalo kwa sasa wataepukana nalo kwa kupata mkopo wa maji usio kuwa na riba kutoka IDYDC.

Sauti ya Wananchi Mangawe

Naye mwenyekiti wa Kijiji cha Mangawe Ernest Matto amesema kuwa shirika la IDYDC limewapunguzia gharama kubwa wananchi wake kuunganishiwa huduma ya maji.

Sauti ya Mwenyekiti

Akizungumzia na Wananchi hao, Meneja wa Mradi wa kusaidia kaya maskini kupata huduma ya kuunganishiwa maji kutoka shirika la IDYDC Ndugu Castory David amesema kuwa Mkopo huo wa maji kutoka IDYDC hauna Riba hivyo wananchi watakaounganishiwa huduma hiyo ya maji wanapaswa kurejesha kwa wakati ili waweze kuwahudumia wananchi wengine wenye uhitaji.