Nuru FM

IDYDC kuwapatia maji ya mkopo wananchi Mikong’wi

29 March 2026, 4:07 pm

Maafisa kutoka Shirika la IDYDC na Viongozi wa Kijiji cha Mikong’wi wakizungumza na wananchi wa Kijiji hicho. Picha na Hafidh Ally

Changamoto wa upatikanaji wa huduma ya maji Katika Kijiji cha Mikong’wi imepelekea Uongozi wa kijiji hicho kuwakaribisha Shirika la IDYDC kuwapatia maji ya Mkopo.

Na Hafidh Ally

Wananchi wa Kijiji cha Mikong’wi Kilichopo Kata ya Kising’a Wilaya ya Iringa Vijijini wameanza mchakato wa kupatiwa Mkopo wa huduma ya maji safi na salama kutoka Shirika la IDYDC Kwa kushirikkiana na IRUWASA.

Wakizungumza na Nuru fm baadhi ya wananchi wa kijiji hicho ambao tayari Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Iringa IRUWASA imeshawafanyia tathmini ya Gharama za maji ambazo zitalipwa na IDYDC wamesema kuwa, kwa kupitia mchakato huo wanatarajia kupata huduma ya maji ambayo kwa muda mrefu wameikosa.

Sauti ya Wananchi Mikong’wi
Castory David kutoka IDYDC akitoa maelekezo kuhusu Maji ya Mkopo watakayopatiwa wananchi wa Mikong’wi.

Wananchi hao wamesema kuwa awali walikuwa wakitumia maji kwenye madimbwi na makorongo ambayo walikuwa wakiyatumia na wanyama jambo lililohatarisha afya zao.

Sauti ya Wananchi Mikong’wi

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Mikongwi Marcus Nassor Mlwale amelishukuru shirika la IDYDC kwa kuwapatia maji hayo ya Mkopo ambapo wananchi wake wanatarajia kunufaika na Maji hayo kwa kufanya kilimo cha Mboga mboga.

Sauti ya Mwenyekiti

Awali Meneja wa Mradi wa kusaidia kaya maskini kupata huduma ya kuunganishiwa maji kutoka shirika la IDYDC Ndugu Castory David amesema kuwa mpaka sasa kuna maombi mengi ya wananchi wa Mikong’wi kutaka huduma ya maji ya Mkopo huku akiiomba Serikali na wadau wa maendeleo kushirikiana nao ili waweze kuwafikia wananchi wengi zaidi na kupata huduma ya maji.

Martin Haule Kutoka Shirika la IDYDC akiwaelekeza wananchi kujaza mkataba wa kupatiwa huduma ya maji ya Mkopo.