Nuru FM

RC kheri ataka mapinduzi ya kifikra kwa wanafunzi

27 March 2026, 7:58 am

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James akizungumza na wakuu wa Shule za Sekondari Mkoani Iringa. Picha na Hafidh Ally

Wakuu wa Shule wameagizwa kusimamia malezi bora kwa wanafunzi ili kuwainua kifikra.

Na Hafidh Ally

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James, amewataka wakuu wa shule za sekondari kuwa mstari wa mbele katika kuleta mabadiliko ya kifikra kwa wanafunzi, akisisitiza kuwa elimu bora siyo tu kuhusu ufaulu wa mitihani bali pia malezi ya maadili na ujuzi unaoendana na dunia ya sasa.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari (TAHOSA) mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri amesema kuwa wakuu wa shule wanayo nafasi ya kipekee ya kuwa chachu ya mabadiliko hayo kwa kuhakikisha mazingira ya kujifunzia yanachochea ubunifu, nidhamu na uwajibikaji.

Sauti ya Kheri

Aidha Mhe. Kheri, amesisitiza kuwa elimu inapaswa kuwajengea wanafunzi uwezo wa kukabiliana na changamoto halisi za maisha na kuwaandaa kuwa raia wenye tija na mchango chanya kwa jamii.

Sauti ya Kheri

Kwa upande wao baadhi ya wakuu wa shule za Sekondari Mkoani Iringa wamesema kuwa watahakikisha wanasimamia kwa weledi na kuwaongezea wanafunzi ubunifu ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya dunia.

Sauti ya Wakuu wa Shule

Kikao hicho cha TAHOSA kimewakutanisha wakuu wa shule kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huu kwa lengo la kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu mbinu bora za kuinua kiwango cha elimu.