Nuru FM

Wezi wa Pikipiki 115 wakamatwa Iringa

26 March 2026, 10:11 am

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa SACP Allan Bukumbi. Picha na Hafidh Ally

Baadhi ya watuhumiwa walikiri kuhusika na wizi wa pikipiki zaidi ya 50 kila mmoja na kubainika kuwa walikuwa wakitengeneza kadi bandia.

Na Hafidh Ally

Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limefanikiwa kuvunja mtandao mkubwa wa wizi wa pikipiki uliokuwa ukifanya uhalifu katika mikoa kadhaa nchini, baada ya kukamata pikipiki 115, watuhumiwa tisa na mali mbalimbali za wizi.

Akizungumza na Wanahabari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi, amesema kuwa operesheni hiyo ilifanyika Januari 17, 2026, katika eneo la Kihesa, Manispaa ya Iringa, na kufanikisha kubaini mtandao uliokuwa ukihusika na wizi katika mikoa ya Dodoma, Iringa, na Morogoro ambapo Watuhumiwa wa awali walikamatwa wakiwa na pikipiki zilizoibwa na walikiri kuiba zaidi ya pikipiki 50 kila mmoja.

Sauti ya Kamanda Bukumbi

Aidha Kamanda Bukumbi amesema kuwa uchunguzi huo uliendelea hadi mji wa Makambako ambako watuhumiwa wengine walikamatwa wakiwa na mali zaidi, ikiwemo pikipiki 82, kadi bandia, na fedha taslimu.

Sauti ya Kamanda Bukumbi

Katika hatua Nyingine Kamanda wa Jeshi la Polisi SACP Bukumbi amesema operesheni hiyo bado inaendelea na amewataka wananchi walioibiwa pikipiki zao kufika Kituo Kikuu cha Polisi Iringa kwa ajili ya utambuzi wa mali zao na kisha kukabidhiwa.

Sauti ya Kamanda Bukumbi