Nuru FM

Iringa yazindua kampeni ya upandaji miti

26 March 2026, 9:02 am

Mstahiki Meya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada akipanda Mti. Picha na Hafidh Ally

Kila nyumba ndani ya Halmashauri inakuwa na mti kwani upandaji wa miti ni kitu bora katika maisha ya binadamu.

Na Hafidh Ally

Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imezindua Kampeni ya upandaji miti iliyopewa jina la “Mti Wangu Nyumba Yangu” ili kukabiliana na changamoto za uharibifu wa mazingira.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo Mstahiki Meya wa Manispaa Mhe. Ibrahim Ngwada amesema kuwa ni vyema wananchi kupanda miti katika makazi yao yanayowazunguka.

Sauti ya Meya Ngwada

Aidha Mhe. Ngwada amawasihi Wenyeviti wa Mitaa yote kuhakikisha kila nyumba ndani ya Halmashauri inakuwa na mti kwani upandaji wa miti ni kitu bora katika maisha ya binadamu.

Sauti ya Meya Ngwada

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Bi. Happiness Nnko amesema katika mwaka wa fedha 2025/2026 Halmashauri imefanikiwa kuzalisha miche ya miti laki nane.

Sauti ya Happiness

Uzinduzi wa kampeni hiyo umefanyika katika Ofisi za Kata ya Mshindo, Manispaa ya Iringa, ambapo wananchi wametakiwa kushiriki kikamilifu katika zoezi la kupanda na kutunza miti ili kulinda mazingira na kuifanya Manispaa ya Iringa kuwa ya kijani na yenye kuvutia.