Nuru FM

Urasimishaji ardhi kupunguza migogoro ya ardhi Iringa

25 March 2026, 10:16 am

Mkuu wa Idara ya Ardhi Halmahauri ya Wilaya ya Iringa Bw. Geofrey Kaluwa akizungumza katika kipindi cha Kiyoyozi kinachoruka Nuru FM. Picha na Telesia Chalamila

Mpango huu unalenga kuhakikisha kila kipande cha ardhi nchini kinapimwa ili kumwezesha mmiliki kuwa na haki mbalimbali zinazoambatana umiliki wa ardhi.

Na Telesia Chalamila

Wananchi wilaya ya Iringa wametakiwa kurasimisha umiliki wa ardhi zao ili kupunguza migogoro ya ardhi na kuongeza thamani yake.

Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa Idara ya ardhi Halmahauri ya Wilaya ya Iringa Bw. Geofrey Kaluwa na kuongeza kuwa hatua za urasimishaji ardhi inasaidia utambuzi wa kipande cha ardhi.

Sauti ya Kaluwa

Naye Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Calist Mushi ameeleza kuwa ni vyema kabla ya wananchi kuuza kiwanja wahakikishe wanapata miongozo kutoka katika vyombo husika.

Sauti ya Calist

Awali Mpima ardhi kutoka Halmahauri hiyo Jesse Josephati amebainisha kuwa maeneo yenye huduma za kijamii kama barabara na hospitali ni moja ya maeneo muhimu ambayo huanza katika utambuzi ili kurasimishwa.

Sauti ya Josephati