Nuru FM

TGNP- Vijana na wanawake shirikini katika Maamuzi

17 March 2026, 4:29 pm

Washiriki wa mafunzo kutoka TGNP. Picha na Joyce Buganda

Mafunzo hayo yamehusisha zaidi ya washiriki 24 kutoka maeneo mbalimbali yakilenga kuwajengea uwezo wanawake na Vijana ili waweze kushiriki kikamilifu katika uongozi katika ngazi mbalimbali za jamii na taasisi.

Na Joyce Buganda

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kupitia mradi wa Ustahimilivu – Wake Dunia Yetu, unaotekelezwa kwa ushirikiano na CARE International umeendesha mafunzo ya kuimarisha ushiriki wa wanawake na vijana wa kike katika nafasi za maamuzi katika jamii.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mwajuma Mkombozi kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) amesema lengo la mafunzo hayo ni kumuwezesha mwanamke kujitambua na kujiamini ili aweze kushika nafasi za uongozi na kushiriki katika kufanya maamuzi yanayohusu maendeleo ya jamii.

Sauti ya Mwajuma

Amesema wanawake na vijana bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazowazuia kushiriki kikamilifu katika uongozi, hivyo mafunzo hayo yamelenga kuongeza uelewa na kuwajengea uwezo wa kujitokeza kugombea na kushika nafasi za uongozi.

Sauti ya Mwajuma

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema yamewasaidia kupata uelewa mpana kuhusu masuala ya uongozi, usawa wa kijinsia pamoja na haki zao, jambo litakalowasaidia kushiriki zaidi katika shughuli za maendeleo na uongozi ndani ya jamii zao.

Sauti ya Washiriki