Nuru FM

Mafuriko yababisha maafa Kijiji cha Makatapola

13 March 2026, 8:34 am

Kamati ya Ulinzi na usalama wakitoa takataka katika daraja ili kurahisisha maji yapite. Picha Ayoub Sanga

Mvua hizo zimesababisha uharibifu wa nyumba, upotevu wa mali pamoja na kuharibiwa kwa mazao yaliyokuwa mashambani.

Na Ayoub Sanga

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali mkoani Iringa zimesababisha maafa makubwa ikiwemo uharibifu wa nyumba, upotevu wa mali na kuharibiwa kwa mazao yaliyokuwa mashambani katika Kijiji cha Makatapola,Kata ya Migoli.

Wakizungumzia maafa hayo baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Makatapola wamesema kuwa kaya 255 zimeathirika na kukosa mahali salama pa kuishi na kulala, huku wakiiomba Serikali kuwasaidia ili waweze kurejesha maisha yao katika hali ya kawaida.

Sauti ya Wananchi
Mkuu wa wilaya ya Iringa Benjamin Sitta akizungumza na wakazi wa Makatapola

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Migoli Bi. Fatma Moge, amewatoa hofu wananchi akisema kuwa licha ya uharibifu wa mali uliotokea, hakuna kifo kilichoripotiwa hadi sasa wakati Serikali ikiendelea kuchukua hatua za haraka kuhakikisha waathirika wanapatiwa msaada unaohitajika kwa wakati.

Sauti ya Diwani Migoli

Nye Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Benjamin Sitta, ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya kuhakikisha wananchi walioathirika na mafuriko katika kijijii cha Makatapola , Kata ya Migori wilayani humo wanapatiwa msaada wa dharura haraka.

Sauti ya DC Sitta