Nuru FM

Wananchi Ibangamoyo wanufaika na maji ya IDYDC

12 March 2026, 8:42 am

Castory David ni Meneja wa Mradi wa kusaidia kaya maskini kupata huduma ya kuunganishiwa maji kutoka shirika la IDYDC akizungumza na wananchi Ibangamoyo. Picha na Hafidh Ally

Mradi huu unatekelezwa lengo likiwa ni kuwalipia maji ya Mkopo kupitia IRUWASA na kisha wananchi kulipa kidogo kidogo.

Na Hafidh Ally

Wananchi wa Mpaka kijiji cha Ibangamoyo Kilichopo Kata ya Ulanda Wilaya ya Iringa Vijini wamenufaika na mradi wa maji ya Mkopo unaotekelezwa na shirika la IDYDC kwa kushirikiana na Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mkoa wa Iringa IRUWASA.

Wakizungumza na Nuru fm mara baada ya kutembelewa na Maafisa kutoka IDYDC kuona utekelezaji wa mradi huo, baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamesema kuwa mara baada ya kufungiwa huduma hiyo ya maji ya mkopo kwa sasa wameepukana na changamoto ya kutumia maji ambayo siyo safi na salama.

Sauti ya Wananchi

Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ibangamoyo amesema kuwa Mradi huu wa maji umeweza kuokoa ndoa za wananchi wake ambao walikuwa wakiamka asubuhi kufuata huduma za maji.

Sauti ya Mtendaji

Awali Mwenyekiti wa Kijiji cha Ibangamoyo Bw. Flomenus  Nyakunga anasema mpaka sasa wanakijiji wake 30 wamepata huduma ya maji ya mkopo kutoka IDYDC kwa kushirikiana na Iruwasa.

Sauti ya Mwenyekiti Ibangamoyo

Castory David ni Meneja wa Mradi wa kusaidia kaya maskini kupata huduma ya kuunganishiwa maji kutoka shirika la IDYDC amesema lengo lao ni kuwapatia huduma ya maji kaya 400 kwa mwaka huu 2026.

Sauti ya Meneja Mradi Castory

Mpaka sasa mradi huo umeweza kuwafikia kaya 150 huku lengo la mradi huo ni kuhakikisha wananchi katika wilaya ya iringa vijijini na Manispaa ya iringa wanapata huduma bora ya maji safi na salama.

Wananchi wa Kijiji cha Ibangamoyo ambao ni wanufaika wa mradi wa maji Kutoka IDYDC na IRUWASA