Nuru FM

Forland wazindua utafiti sekta ya misitu Iringa

11 March 2026, 9:27 am

Mkuu wa Mkoa wa Iringa akizungumza katika kikao cha kupokea utafiti sekta ya Misitu. Picha na Joyce Buganda

Utafiti huo wa sekta ya misitu unatarajia kukuza mnyororo wa thamani ya mazao hayo kwa wakulima wadogo.

Na Joyce Buganda

Serikali Mkoani Iringa kwa kushirikiana na Shirika la Forland Tanzania imezindua matokeo ya utafiti kuhusu maendeleo ya sekta ya misitu, huku ikiweka msisitizo kwenye kujenga mazingira mazuri na wezeshi yatakayowawezesha wakulima wadogo wa miti kushiriki kikamilifu katika mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu.

Akifungua kikao maalum cha kupokea matokeo ya utafiti huo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amesema utafiti huo umefanyika katika kipindi ambacho Serikali inaendelea kuweka msukumo wa kuboresha mazingira ya sekta ya misitu, huku pia ikiwapa kipaumbele wakulima wadogo wa miti kwa kuwaangazia kwa mtazamo wa kipekee ili waweze kunufaika zaidi na fursa zilizopo katika sekta hiyo.

Sauti ya RC Kheri

Naye Mtafiti na Mshauri Elekezi kwenye sekta ya misitu  Ignatus Matofari amesema  sekta hiyo inakabiliwa na changamoto hasa uchakataji na usindikaji wa mbao pamoja na wakulima kutawaliwa na madalali Jambo ambalo linamkandamiza mkulima.

Sauti ya Mtafiti

Kwa upande wao ubalozi wa Finland wamesema waliona wafadhili mradi huo kwa sababu wao ni wadau wa misitu pia wanatamani mapendekezo yaliotolewa yakafanyiwe kazi ipasavyo, wameongeza na kusema wanatarajia kuwanufaisha wakulima walime kwa tija.

Sauti ya Ubalozi

Utafiti huo wa sekta ya misitu na mnyororo wa thamani ulihusisha wakulima wadogo 214 wa miti wa mkoani Iringa na ulifanywa na FORLAND kwa ufadhili wa ubalozi wa FINLAND na warsha hiyo ilihudhuliwa na wakuu wa wilaya za kilolo, Mufindi, Iringa, Wenyeviti wa Halmashauri zote na wakurugenzi wote wa wilaya hizo.