Nuru FM

Wanawake Iringa DC watoa msaada kwa watoto

8 March 2026, 8:00 am

Wanawake Iringa DC wakitoa msaada katika vituo vya watoto wenye uhitaji. Picha na Joyce Buganda

“Tumeona tusherehekee siku ya wanawake duniani Kwa kutoa msaada wa mahitaji Kwa watoto hawa”

Na Joyce Buganda

Wanawake kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wameadhimisha maadhimisho ya siku ya wanawake kiwilaya kitofauti kwa kwenda kutembelea vituo viwili vya watoto yatima ambavyo ni kituo Cha watoto yatima Asante sana kilichopo kata ya nzihi na kituo Cha watoto yatima Tosamaganga ambavyo vyote vipo katika Wilaya ya Iringa.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vitu mbali mbali katika vituo hivyo Mkuu wa idara ya maendeleo ya Jamii Wilaya ya Iringa Bi Saumu Kweka amesema mwaka huu wameona wafanye kitofauti kwa kwenda kuwaona watoto wenye uhitaji pia amewaasa wanawake kuwa na utaratibu wa kwenda kutembelea vituo hivyo kwani kwa kufanya hivyo kunafanya watoto wajisikie faraja.

Sauti ya Saumu

Kwa upande wao viongozi na wasimamizi wa vituo hivyo wamewashukuru wanawake hao kwa kujitoa kwao kwenda kuwaona na kuwasaidia mahitaji mbali mbali.

Sauti ya Msimamizi Kituo

Pamoja na hayo wanawake wa Halmashauri hiyo walifanya kongamano kubwa la wanawake katika ukumbi wa siasa ni kilimo huku mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Benjamin Sitta.