Nuru FM
Nuru FM
7 March 2026, 10:41 am

Kliniki hii ina lenga kuhakikisha wanawake wanapata fursa ya kumiliki ardhi sawa na wanaume.
Na Telesia Chalamila na Elika Matonya
Kuelekea maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Wizara ya ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Ofisi ya ardhi Mkoa wa Iringa imeandaa kliniki maalumu ya ardhi ijulikanayo kama samia ardhi kliniki kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto za ardhi zinazowakabili wananchi hususani wanawake.
Akizungumza na Nuru FM Josefer Mwenda Msajili wa ardhi Msaidizi Mkoa wa Iringa amesema kuwa Samia Ardhi Kliniki imeandaliwa rasmi kwa lengo la kutatua migogoro ya ardhi ikiwa ni pamoja na masuala ya umiliki wa hati.
Bi Flora shija Afisa ardhi Mkoa ameeleza kuwa wameamua kuweka kliniki ya ardhi kwa lengo la kusaidia kukuza ongezeko la wanawake wanao miliki hati Tanzania na pia ameshauri jamii kwa ujumla kuzingatia haki na usawa.

Nae mnufaika katika kliniki hiyo, Bi Tusajigwe Emmanuel na mmiliki wa ardhi Manispaa amesema kuwa amenufaika na kliniki hiyo kwani ameishi mda mrefu bila hati lakini kupitia Samia ardhi kliniki imemsaidia kuwa mmiliki halali wa eneo lake.
