Nuru FM
Nuru FM
6 March 2026, 4:02 pm

“Maadili bora katika jamii yanaanzia kwa wanawake hivyo wanapaswa kuwa mstari wa mbele”
Na Joyce Buganda
Wanawake wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wametakiwa kusimamia maadili mema na malezi katika familia zao na jamii inayowazunguka.
Akizungumza wakati wa kufunga kongamano la Siku ya wanawake wa Manispaa ya Iringa liliofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari lugalo kamishina wa ardhi mkoa wa Iringa Bi Rehema Kilonzi ambae ndiye alikuwa mgeni rasmi wa kongamano hilo amewaasa wanawake kuonyesha uwezo wa kimaadili pale wanapopata nafasi ili waonekane na kupewa kuongezewa fursa katika ngazi mbalimbali.

Zaina Mlawa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wanawake wana uwezo mkubwa wa kuongoza kwaiyo wanawake wanatakiwa kuwa na nidhamu kuanzia kwenye familia mpaka jamii inayowazunguka.
Kwa upande wake Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Iringa Mjini Jesca Msambatavangu amewataka wanawake kusimama imara katika mambo yao kupambana na changamoto za kazi, ndoa pia kusaidiana katika jamii zao.
Halmashauri ya manispaa ya Iringa itafanya maadhimisho yao tarehe 7 mwezi wa 3 katika viwanja vya samora na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Benjamin Sitta.