Nuru FM
Nuru FM
5 March 2026, 6:36 pm

Uzinduzi wa kadi alama utasaidia kupata takwimu sahihi na kujua namna bora ya kulea na siyo kutunza watoto.
Na Hafidh Ally
Maafisa wanaotekeleza Afua tano za mradi wa Program Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto PJT-MMMAM Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wameahidi kutumia mafunzo ya matumizi ya Kadi ya alama (SCORECARD) kwa vitendo katika ufuatiaji wa maendeleo ya makuzi na malezi ya watoto.
Wakizungumza Mara baada ya kupatiwa mafunzo ya namna bora ya kutumia Kadi ya Alama yaliyoratibiwa na Mtoto Kwanza kupitia Shirika la Developmentof Youth Disable and Children Care (IDYDC), Baadhi ya Maafisa Ustawi wa Jamii, Afisa elimu, Afisa afya wa Halmashauri ya Wilaya hiyo walisema kuwa kuna namna mtoto anapaswa kuandaliwa vyema kuanzia kipindi cha ujauzito, unyonyeshwaji na malezi kwa ujumla.
Naye Mkufunzi wa mafunzo hayo ambaye pia Afisa Ustawi wa Jamii Bw. Hamza Shemweta amesema kuwa matarajio yao ni kuona Maafisa hao wanajua namna bora ya kuandaa taarifa sahihi ili jamii iweze kujua maendeleo ya makuzi na malezi katika kuzingatia afya ya mzazi/Mlezi na mtoto.
Awali Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Iringa na Mratibu wa PJT–MMMAM Martine Chuwa amesema kuwa jukumu la malezi ni la wote huku akiwataka wanaume kushiriki ipasavyo ili kuwa kizazi chenye maadili yanayokubalika katika jamii.
Tukuswiga Mwaisumbwe ni Mwanahabari Mchechemuzi wa habari za Watoto Mkoani Iringa ameshauri Watoto wenye mahitaji maalumu wasiachwe kwenye Mfumo wa Kadi alama ili kupata takwimu zao sambamba na wanaume kushirikishishwa katika Malezi Bora ya watoto katika famili.
Hata hivyo wataalamu walikumbushwa kuwa Takwimu wanazozitoa wanapaswa kuzitolea maoni Katika nyanja ambayo Bado Kuna Changamoto katika Utekelezaji wake ili kusaidia kutokomeza kabisa changamoto hizo.
