Nuru FM

Ngajilo aibana serikali daraja la Isakalilo-Kitwiru

28 January 2026, 1:14 pm

Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Fadhili Ngajilo akiuliza swali bungeni Jijini Dodoma.

“Daraja hilo limekuwa muhimu kwa wananchi wa eneo hilo hivyo tunaomba Mradi utekelezwe kwa full package”

Na Hafidh Ally

Serikali imeahidi kuanza utekelezaji wa ujenzi wa Daraja la Isakalilo-Kitwiru lilopo kwenye barabara hiyo yenye urefu wa KM 3.

Hayo yamezunguzmwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Mh. Rubein Kwagilwa wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mh.  Fadhili Fabian Ngajilo Aliyetaka kujua ni lini daraja la isakalilo-Kitwiru litajengwa ili kufungua utalii wa mbuga ya wanyama Ruaha?

Sauti ya Kwagilwa
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEM Mh. Rubein Kwagilwa akijibu swali Bungeni

Katika swali la Nyongeza, Mh. Ngajilo amehoji kwa zaidi ya miaka 20 wananchi walihoji kuhusu barabara hiyo na kuiomba serikali itoe majibu ya lini ujenzi huo utaanza?

Sauti ya Ngajilo

Akijibu swali hilo, Naibu waziri huyo amesema kuwa tayari serikali imeshatenga zaidi ya Bilioni 2 kwa ajili ya mradi huo na umeshaanza kutekelezwa kwa awamu ya 1.

Sauti ya Kwagilwa