Nuru FM
Nuru FM
28 January 2026, 12:48 pm

Nyumba hii itasaidia viongozi wa jumuiya hii kukaa sehemu salama na kutekeleza majukumu ya Chama.
Na Fredrick siwale
Mjumbe wa mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mufindi Ndg. Dickison Mwipopo ameahidi kugharamia umaliziaji wa ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Jumuiya hiyo.
Akifungua Kikao cha Jumuiya ya Wazazi Wilaya Ndg. Dickison Mwipopo, amesema atagharamia kwa kutoa mbao za upauaji, mabati na kupiga lipu jengo hilo ambalo limefikia hatua ya Boma.

Ndg. Mwipopo amewataka Wazazi Wilayani humo kujenga tabia ya kuwalea Watoto wao katika malezi bora ili kuwaepusha na matukio ya ukatili kwa faida ya Jamii na Taifa kwa ujumla.
Awali Aidha akitoa semina Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Iringa Bi. Rehema Mbedule alionyesha kusikitishwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii ikiwemom wanawake kuwapiga waume zao.
Amesema kuwa matukio ya wanaume kupigwa na wake zao yameripotiwa zaidi jambo ambalo wanaungana na mamlaka nyingine kukemea.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Ndg. Festo Kilipamwambu alimshukuru Mgeni rasmi Ndg. Mwipopo kwa kuwa na moyo wa Uzalendo na vitendo kwa chama cha Mpinduzi CCM.
