Nuru FM

Wananchi Kitasengwa walalamikia ubovu wa barabara

26 January 2026, 11:39 am

Wananchi wa Kitasengwa wakitoa kero kwa Mbunge Fadhili Ngajilo. Picha na Hafidh Ally

Ubovu wa miundombinu ya barabara katika eneo la Kitasengwa, Manispaa ya Iringa, imeendelea kuwa kero kubwa kwa wananchi

Na Hafidh Ally

Wananchi wa Kitasengwa Kata ya Isakalilo Manispaa ya Iringa wanakabiliwa na changamoto ya miundombinu ya barabara inayotajwa kuwa kero kwa wagonjwa, wajasiriamali na wajawazito.

Wakizungumzia kero hiyo wananchi hao wamesema kuwa eneo la Kitasengwa linakikabiliwa na adha kubwa ya ubovu wa barabara hasa jambo linalopelekea mama wajawazito kujifungulia njiani pindi wanaposafiri kufuata huduma za afya.

Sauti ya Wananchi

Aidha wananchi hao wamesema kuwa kuna changamoto pia ya barabara za mitaa na kuongeza kuwa serikali ikianza kufanya maboresho ya miundombinu ya barabara wasisahau pia kuwapatia huduma ya umeme.

Sauti ya Wananchi

Akitolea majibu ya kero hiyo mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mh. Fadhili Fabian Ngajilo amesema ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko mengi kuhusu barabara hiyo huku akiahidi akianza kuchukua hatua za kuwasiliana na mkandarasi wa ujenzi wa Barabara hiyo.

Sauti ya Ngajilo

Ngajilo amesema kuwa tayari mkandarasi ameshalipwa fedha za ujenzi wa Barabara hiyo itakayoenda sambamba na ujenzi wa mifereji huku akiahidi yeye pamoja na ofisi yake kufuatilia kwa karibu ujenzi huo.

Sauti ya Mbunge