Nuru FM
Nuru FM
15 January 2026, 12:25 pm

Bodi ya Copra imelenga kuhakikisha wakulima wanalima kisasa na kuvuna mavuno mengi.
Na Hafidh Ally
BODI ya Mazao ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) imekabidhi KG 500 za mbegu bora za mbaazi kwa wakulima wadogo wa mkoa wa Iringa kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Kilimo katika kuhamasisha kilimo cha kisasa cha zao la mbaazi.
Afisa Kilimo wa COPRA Nyanda za Juu Kusini, Edwin Magwe, amesema mbegu hizo ni matokeo ya utekelezaji wa mfumo wa stakabadhi ghalani, unaolenga kuongeza uzalishaji wa zao la mbaazi, kuboresha ubora wa mazao na kuongeza tija kwa wakulima.
Aidha Magwe amesema kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza uzalishaji na tija ya zao hilo la kimkakati ambalo limeendelea kuwa na soko zuri la ndani na nje ya nchi.
Akipokea mbegu hizo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amesema Mkoa wa Iringa umeendelea kuyapa kipaumbele mazao ya kimkakati, yakiwemo mbaazi, kwa lengo la kuwavuta wakulima wengi zaidi kushiriki katika kilimo cha zao hilo na kuongeza uzalishaji pamoja na kipato cha wananchi.
Matokeo ya juhudi hizo yanatarajiwa kuwa na mchango Chanya kwenye uchumi wa wakulima na Taifa kwa ujumla.