Nuru FM
Nuru FM
21 December 2025, 12:46 pm

“COP 30 imekuwa na manufaa kwa wakulima kwani wanalima kisasa”
Na Joyce Buganda
Siku chache baada ya wakulima kuwa na uelewa kuhusu mkutano wa umoja wa mataifa wa mabadiliko ya tabia nchi COP 3O mashirika mengi yameanza kutoa miradi ya kilimo ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayotokea kila mwaka.
Irene Mobito mkufunzi wa Kilimo kutoka Shirika Campain for Female Education CAMFED anasema lengo la kuwa na mradi huo wa kilimo ni kuwafundisha wasichana wanaofadhiliwa na Shirika lao kuandaa mazao ambayo yanakabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kukuza uchumi wao.
Kwa upande wao baadhi ya wasichana walionufaika na mradi huo wamesema wanavyopata mafunzo tofauti ya kilimo wanajikuta wakipenda kulima mazao mbalimbali kama mbogamboga ambayo inawasaidia kwenye lishe.
Mkutano wa umoja wa mataifa wa mabadiliko ya tabia nchi kwa mwaka huu umefanyika katika mji wa Belem nchini Brazil ambapo Tanzania kama mwanachama wa umoja wa mataifa iilipeleka agenda 12 ambazo zilijadiliwa.