Nuru FM
Nuru FM
8 December 2025, 8:49 pm

Kauli mbiu ya Mahakama ya Tanzania Kanda ya Iringa inasema siku zote ni uadilifu ueledi na uwajibikaji.
Na Joyce Buganda
Ikiwa tupo katika wiki ya maadhimisho ya miaka 20 ya mahakama Kuu Tanzania kanda ya Iringa, Wananchi Mkoani Hapa wametakiwa kujifunza mambo ya kisheria, haki na kimahahama.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Kheri James amesema maadhimisho hayo yanaanza Leo tarehe 8/12/2025 kwa kuanza na vipindi vya radio na televisheni na kilele chake kitafanyika 15/12/2025.
Rc kheri amesema umuhimu wa miaka 20 kwa kanda ya Iringa ni ushuhuda safari ndefu wa kazi zinazofanyika kama kurahisisha utendaji kazi wa kimahakama, matumizi ya tehama kuongeka kwa majaji na watumishi.

Hata hiyo DC kheri amesema mahakama serikali imeendelea kushirikiana na mahakama kama muhimili wa dola masuala ya kiusalama miundombimu , kutoa maeneo ya ujenzi wa vituo vya mahakama ya mwanzo katika mkoa wa Iringa hiyo yote ni kwa mujibu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania