Nuru FM
Nuru FM
5 December 2025, 11:45 am

Mwongozo wa uwazi utasaidia kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika Jamii na kukuza uwajibikaji kwa wakulima.
Na Joyce Buganda
Mkutano wa COP 30 umefanikiwa kuweka muongozo wa wazi katika masuala ya fedha na kuongeza uwajibikaji wa mataifa yalioendelea katika kutekeleza ahadi zao mfuko wa mabadiliko ya tabianchi umeahidi kuimarisha upatikaji wa fedha kwa nchi tajiri.
Hayo yamezungumzwa na mkurugenzi wa sera za tabia nchi kutoka Tanzania policy Bi Rehema Mzena na Kuongeza kuwa makubaliano hayo yamefungua rasmi ukurasa mpya kupitia miradi ya kijani , ulinzi wa ikolojia na nishati.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya ENVRIBRIGHT inayojishughulisha na kilimo na mazingira Paul Myovela amesema ni vyema wakulima wakawajibika ipasavyo kwa kufuatilia yale yaliojadiliwa huko kwenye mkutano wa COP 30 ili iwaletee tija katika kilimo na kutunza mazingira.
Kwa Upande wao baadhi ya Wakulima katika Wilaya ya Iringa wanaonyesha matarajio mapya katika kufanya killimo chao kuwa cha tija zaidi hasa kuelekea katika mkutano mwingine wa COP 31 utakaofanyika mwakani 2026.
Wachambuzi wanasema COP 30 imefungua ukurasa mpya kwenye mijadala ya kijinsia na tabianchi utekelezaji dhamira ya nchi wanachama bila mifumo ya uwajibikaji na kwa bajeti mahususi kwa uwakilishi wa wanawake na maadhimio hayo yanaweza kubaki kwenye kumbukumbu katika mikutano mingine.