Nuru FM
Nuru FM
3 December 2025, 1:43 pm

“Ukusanyaji wa mapato utasaidia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo”
Na Fredrick Siwale
Madiwani wa Baraza jipya la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, wamekula kiapo cha utii na uwajibikaji kwa kipindi cha mwaka 2025 hadi 2030.
Kiapo hicho kimesimamiwa na Mhe. Benedict Nkomola, mbele ya Dkt. Linda Salekwa Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Bw. Ruben Chongolo Katibu Tawala wa Wilaya na Mashaka mfaume Mkurugenzi Mtendaji wa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.

Baada ya kiapo hicho Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Dkt. Linda Salekwa , amewataka Waheshimiwa Madiwani hao kwenda kuwaletea Wananchi maendeleo kwa kuibua vyanzo Vipya vya mapato.
Dkt. Salekwa amesema ufike wakati ambao fedha za mapato za Vikundi na maendeleo yake zipatikane kupitia miradi mipya inayobuniwa tofauti na ilivyo hivi sasa.

Akizungumza baada ya kula kiapo cha Utiifu Diwani wa Kata ya Makungu Felix Lwimbo amesema kuwa atahakikisha anafanya kazi kwa bidii kuwatumikia wananchi kwani tayari amesimamia utekelezaji wa miradi ya Bilion 5.6 katika kata yake.