Nuru FM
Nuru FM
2 December 2025, 11:35 am

“Changamoto ya Barabara inatakiwa kutatuliwa ili kukuza uchumi wa wananchi wa Kilolo”.
Na Hafidh Ally
Mbunge wa jimbo la Kilolo, Dr. Ritta Kabati amefanya ziara ya kikazi katika ofisi za wakala ya barabara za vijijini na Mijini (TARURA) wilaya ya Kilolo ili kupata taarifa za miradi inayoendelea na hatua ilikofia.
Ziara hiyo imelenga kupata taarifa za miradi inayoendelea katika wilaya ya Kilolo huku Mh. Kabati akisema kuwa barabara za kilolo hazipitiki katika kipindi cha mvua na wameahidi kushirikiana kutatua changamoto hizo.

Aidha Dkt. Kabati amesema kuwa kuna matengenezo ambayo yameanza kufanyika katika barabara zenye changamoto na lengo ni kuhakikisha Kilolo inakua kiuchumi.
Kwa upande wake Katibu wa siasa uenezi na mafunzo wa CCM Wilaya ya Kilolo Reminius Valentino Sanga amesema kuwa wameona mipango mizuri kutoka Ofisi ya TARURA Wilaya na wameridhika nayo katika utekeleaji ili kuorodhesha barabara zenye changamoto hususani katika kipindi hiki cha mvua ili kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu.