Nuru FM

Wakulima Iringa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

24 November 2025, 10:04 pm

Moja ya shamba wilayani Kilolo likiwa kwenye maandalizi ya kilimo. Picha na Joyce Buganda

Wananchi wanakumbushwa kudumisha uhifadhi wa mazingira huku wakichukua hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Na Joyce Buganda

Nuru FM imekuandalia makala fupi kuhusu mkakati wa serikali mkoani Iringa wenye lengo la kuwaunganisha wananchi katika mifumo na miradi ya pamoja ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, hususan kwa wakulima wanaohitaji mbinu bora na kilimo chenye tija.