Nuru FM

COP 30 kuleta mabadiliko kwa wakulima Iringa

9 November 2025, 2:18 pm

Afisa Mazingira mkoa wa Iringa Golyama Bahati akieleza mabadiliko ya tabia nchi yanavyoathiri wakulima. Picha Joyce Buganda

Tanzania ni mwanachama wa mkataba wa umoja wa mataifa na mabadiliko ya tabia nchi, itifaki ya Kyoto na makubaliano ya Paris UNFCCCTanzania ikiwa kama mshiriki wa mkutano wa COP 30.

Na Joyce Buganda

Wataalamu wa masuala ya mazingira wametakiwa kuwafikia wananchi na kuwapatia elimu ya mabadiliko ya tabia nchi ili kuwasaidia kukabiliana na changamoto zitakazo jitokeza hasa katika nyanja ya kilimo na kutunza mazingira hasa katika kipindi hiki cha kuandaa mashamba na kuelekea mkutano wa COP 30.

Tanzania inaungana na nchi zingine kushiriki mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya hali hewa unaojulikana kama COP 30 ambao unatarajia kuanza Novemba 10 mpaka 20 katika mji wa Belem nchini Brazil, huku Tanzania ikiwa kama mwanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi inakwenda na kauli mbiu isemayo Dira ya 2050;Utekelezaji wa  hatua jumuishi za ustahimilivu wa mabadiliko ya tabianchi.

Mkakati wa sera ya mazingira ni kutoa elimu ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira ambayo inaambatana na matukio kama mikutano ya kimataifa kujadili mabadilko ya tabia nchi, Pia kuifanya ajenda ya mazingira kuwani ya kitaifa na  ni jukumu la kila mmoja kuanzia ngazi ya familia, kuna sheria na sera za katika sekta ya maji  toleo la 2025 sheria namba 5 ya mwaka 2019 ya huduma ya maji na usafi wa mazingira.

Afisa Mazingira Mkoa wa iringa Dkt. Golyama Bahati Akizungumza na Nuru FM anasema kuwa wataalamu  hao watawasaidia wakulima kuwapa maelekezo kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ili kuepukana zitakazo jitokeza.

Sauti ya Goliama

Afisa Kilimo wa Mkoa wa Iringa Bi Rose Kasole anasema mkutano wa COP 30 utakuwa msaada kwa wakulima na wadau wa mazingira kwa ujumla kutambua njia za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi huku wakulima wakitakiwa kulima mazao mchanganyiko ili wasihangaike pindi athari kubwa zinapokea.

Sauti ya Rose

Kwa upande wao baadhi ya wakulima Manispaa ya Iringa wanasema hawakuwa na uelewa wowote kuhusu mkutano huo wa COP 30 ila kwa sasa wataelekeza macho na masikio yao huko nchini Brazil kufuatilia kwani awali walikuwa wakilima kilimo cha mazoea na kusikiliza utabiri wa hali ya hewa jambo ambalo liliwafanya wakati mwingine kupata athari nyingi katika shughuli zao za kilimo

Sauti ya Wakulima

COP 30 ni jukwaa rasmi la kimataifa kwa ajili ya kujadili na kuamua malengo ya kukataa uzalishaji wa hewa ukaa, utunzaji wa mazingira, kutafuta ufadhili wa fedha za kukabiliana na madhara  ya mabadiliko tabianchi na kufikia makubaliano ya kimataifa na sera za kitaifa za mkutano huu na muendelezo wa mikutano inayofanyika kila mwaka kuanzia mwaka 1995 ni majukwaa ya muhimu ambayo lengo kubwa nikuweka mikakati na hatua za pamoja za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.