Nuru FM

Madereva waaswa kuzingatia weledi

23 October 2025, 11:29 am

Kamanda Bukumbi akizungumza na madereva waliohitimu mafunzo katika chuo cha Veta Iringa. Picha na Adelphina

“Udereva ni taaluma kama taaluma nyingine na ni vyema wakazingatia weledi wanaootekeleza majukumu yao”

Na Adelphina Kutika

Madereva wa Magari ya Masafa marefu ndani na nje ya Tanzania wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia msingi kama ya Jeshi la Polisi ambayo ni Nidhamu, Haki, Weledi na Uadilifu ili iwe msingi mafanikio yao kazini.

Hayo yamezungumzwa na Kamanda wa Jesho la Polisi Mkoa wa Iringa, SACP. Allan Bukumbi wakati akizungumza na Wanafunzi wa Udereva wa Magari ya Masafa marefu ndani na nje ya Tanzania waliopo katika mafunzo maalum yanayofanyika Chuo cha VETA Mkoani Iringa, ambapo amesisitiza ili kuongeza weledi.

Sauti ya Kamanda
Madereva wakimsikiliza Kamanda Bukumbi.

Aidha Kamanda Bukumbi amewapongeza wahitimu hao wa udereva na kuwataka kuendelea kushirikiana na Chuo cha Veta na jeshi la Polisi ili wapate ujuzi utakasoaidia kutekeleza majukumu yao.

Sauti ya Kamanda

Naye Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa SP. Glory Mtui, amewataka madereva hao waelewe kuwa Udereva ni Taaluma inayoongozwa na kusimamiwa kwa mujibu wa taratibu, miongozo na sheria za Usalama barabarani.

Sauti ya Mtui