Nuru FM
Nuru FM
23 October 2025, 10:25 am

Na Noela Nyalusi
Jeshi la Polisi Kikosi Cha usalama Barabarani Mkoa wa Iringa limewataka abiria wanaosafiri kwenda mikoani kukata tiketi katika kampuni husika ili kuepuka kulipa kiasi kikubwa tofauti na bei elekezi.
Hayo yamezungumwa na Afisa Usalama barabarani wilaya ya iringa Koplo Elizabeth na kuongeza kuwa kila abiria anatakiwa kujua haki na wajibu wake wakati kusafiri ili kuepuka changamoto zinazojitokeza wakati wa safari.
Aidha Koplo Elizabeth amesema kuwa Abiria anapaswa pia kukemea vitendo hatarishi kwa madereva wanaoendesha gari kwa mwendokasi.
Kwa upande wake Koplo Fadhili amesema abiria ana haki ya kupewa usafiri mbadala endapo chombo kitakuwa kimepata changamoto wakati wa safari ndani ya masaa mawili.
